Muongozo wa Rais Magufuli Kuhusu mifuko ya Hifadhi ya Jamii NSSF

Share:
Muongozo wa Rais Magufuli Kuhusu mifuko ya Hifadhi ya Jamii NSSF

1. Uboreshaji daftari la wastaafu.(Wastaafu hewa)
2. Kupunguza matumizi ya hovyo ya mifuko.(Uchapishaji wa kalenda, huduma mbali mbali Mf. Ulinzi nk)
3. Uwekezaji usio na tija usifanyike. Mf. Dege Village
4. Tupunguze gharama za uendeshaji wa mifuko.
5. Tuongeze Idadi ya Wanachama. Kila anayestahili uanachama ni lazima awe mwanachama.
6. Fao la muda mfupi/kujitoa lirudishwe.

*Uamuzi wa Rais kuhusu Kikokotoo.*

Kwanza Kustaafu sio dhambi. Mtu aliyetumikia Taifa kwa uadilifu ni lazima astaafu kwa furaha.

Tuwe na kipindi cha mpito.

Kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya kuunganisha mifuko kiendelee ndani ya kipindi cha mpito hadi 2023.

Baada ya hapo utafutwe best formula kwa kushirikiana na Wadau wote kwa manufaa ya pande zote (Watumishi VS Waajiri)

No comments